Msanii wa Tanzania Chege Chigunda amepata mtoto wa kike

MSANII Mkongwe wa Bongo Fleva, Saidi Juma Hassani maarufu kama Chege Chigunda amepata mtoto wa kike baada ya mkewe anayefahamika kwa jina la Zahra kujifungua salama salimin jana. Mkali huyo wa ngoma ya KAITABA amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kuweka picha na mkewe huyo na kui-tag akaunti mpya ya mwanaye huyo aliyempa jina la Jadah.