Je, Diamond na Wema wamerudiana!?

Baada ya wawili hao kuwachana miaka kadhaa iliyopita ni dhahiri shairi  kuwa  bado wanapendana. Wema sepetu kupitia kwa ukurasa wake wa instagram aliposti video akiucheza ngoma mpya ya Diamond African beauty aliyomshirikisha Omarion, Msanii huyo wa Wcb aliandika chini ya posti hiyo ya wema kuwa anakubali video hiyo na picha za Wema.isitoshe, Wema ameposti ua la Rose na kusema kuwa ua hilo ni ishara ya mapenzi.

Wakati Zari aliwachana na Diamond, aliposti ua jeusi na sasa hivi Wema ameuposti ua jekundu. je kulikoni?